Subscribe:

Ads 468x60px

Asamoah Gyan astaafu Ghana!



Straika wa Ghana Asamoah Gyan inasemekana ameamua kupumzika kuichezea Ghana baada ya kutuma barua kwa Chama cha Soka Ghana, GFA, akielezea uamuzi wake huo.
Gyan, Miaka 26, ambae ameichezea Ghana mara 59, ameleza kuwa uamuzi wake huo unatokana na kukashifiwa vibaya mara baada ya Ghana kubwagwa nje toka kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2012, hivi majuzi walipofungwa bao 1-0 na Zambia.
Mchezaji huyo amekuwa akisakamwa mno Nchini kwao kwa kuwaletea maudhi makubwa kwa kukosa penati kwenye mechi ya AFCON 2012 dhidi ya Zambia na pia kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay huko Afrika Kusini Mwaka 2010.
Barua hiyo ya Gyan imeeleza kuwa uamuzi wake hakuuchukua kwa mzaha na anasikia fahari kubwa kuichezea Ghana tangu akiwa na Miaka 17 Mwaka 2003.
Akimalizia barua yake, Gyan, ambae sasa anacheza kwa mkopo huko UAE na Klabu ya Al Ain toka Sunderland, amesema ataijulisha GFA akiamua kurudi tena kuichezea Ghana.
Gyan ameifungia Ghana bao 28 katika Mechi 59 alizoichezea.

No comments:

Post a Comment