Subscribe:

Ads 468x60px

WAGHANA HAWANA SHUKRANI...

Emmanuel agyemang Badu


Ikiwa ni siku moja tu tangu mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana,Asamoah Gyan atangaze kustaafu soka la kimataifa,mchezaji mwenzie katika timu ya taifa ambaye anachezea Udinese ya Italia Emmanuel agyemang Badu amesema waghana hawaheshimu juhudi zinazofanywa na wachezaji wa Black Stars
Akiongea na mtandao wa footy-ghana.com,Badu amesema kashtushwa sana na taarifa za kustaafu kwa Gyan na pia amesikitishwa na kitendo cha washabiki wa Ghana kuimiminia matusi makali familia ya Gyan tangu baada ya tukio la kukosa penati kwenye michuano ya kombe la mataifa ya afrika
"matusi yamezidi,waghana hawatambui mchango wa Gyan katika timu ya taifa,yeye ndie mfungaji anaeongoza katika timu yetu,hivyo hii ni habari mbaya kwa Ghana.Familia yake haikustaili matusi yote hayo"

No comments:

Post a Comment