Subscribe:

Ads 468x60px

CAF AFRIKA: Yanga v Zamalek; Kiyovu v Simba

YANGA_V_SIMBA11Klabu kongwe Nchini, Yanga na Simba, Leohii zinajimwaga dimbani kwenye Mashindano makubwa Barani Afrika huku Yanga wakiikaribisha Zamalek ya Misri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo Jumamosi kwa pambano la Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Simba kucheza ugenini, pia Jumamosi, huko Kigali, Rwanda na Kiyovu kwenye Kombe la Shirikisho.
Mbali ya wakongwe hawa, Timu za Zanzibar, Mafunzo na Jamhuri, nazo zitaingia uwanjani kwa Mafunzo kucheza na Liga Muculmana de Maputo ya Msumbiji katika CAF CHAMPIONZ LGI na Jamhuri kuivaa Hangwe ya Zimbabwe kwenye Kombe la Shirikisho.
Tayari Zamalek, ambao wamewahi kuwa Mabingwa wa Afrika mara 5, wameshatua Dar es Salaam bila ya Wachezi wao Ahmed Hassan, Muhammad Ibrahim na Salah Suleiman.
Majuzi Zamalek walicheza mechi yao ya mwisho ya majaribio na kuifunga Telecom Egypt bao 4-1 kwa bao za Amr Zaki, Ibrahim Hassan na Ahmad Jaffar.
Simba yaenda Rwanda bila Wachezaji kadhaa
Simba iliondoka Alhamisi jioni kwenda Kigali, Rwanda kupambana na Kiyovu huku Wachezaji kadhaa wakiachwa.
Wachezaji ambao hawakusafiri ni Gervais Kargo, Derrick Walulya, Haruna Moshi 'Boban', Ulimboka Mwakingwe, Amir Maftah na Hassan Khatib na imesemwa baadhi yao ni majeruhi.
Pamoja na Kocha Cirkovic Milovan na Wasaidizi wake Amatre, Daktari Cosmas Kapinga na James Kisaka, Kocha wa Makipa, Viongozi wengine ambao wamo kwenye msafara huo ni Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange 'Kaburu', Katibu mkuu Evodius Mtawala, Fransis Silaya (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji).
Wachezaji waliosafiri ni:
Makipa: Juma Kaseja na Ali Mustapha 'Barthez'
Mabeki: Nassor Said 'Cholo', Juma Jabu, Juma Nyoso, Kelvin Yondan, Victor Costa na Obadia Mungusa.
Viungo: Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Patric Mafisango Washambuliaji: Ramadhani Singano 'Messi', Edward Christopher, Salum Machaku, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Emmanuel Okwi.

No comments:

Post a Comment