Subscribe:

Ads 468x60px

Edwin van der Sar leo Kiroho papo na kisebusebu!


Leo Edwin van der Sar roho yake imegawanyika mara mbili kwa ajili ya pambano la EUROPA LIGI kati ya Ajax Amsterdam na Manchester United litakalofanyika Uwanja wa Amsterdam ArenA huko Holland.
Kipa huyu stadi ambae yuko kwao Uholanzi baada ya kustaafu mwishoni mwa Msimu uliopita akiwa Manchester United baada ya kuichezea Miaka 6 jana alikwenda kuwaona Man United wakifanya mazoezi Uwanja wa Amsterdam ArenA.
Van der Sar aliongea: ‘Ni vyema nimewaona wenzangu. Nilikuwa na wakati mzuri mno nilipokuwa Man United kwa Miaka 6, huwezi kusahau hilo!’
Lakini Edwin van der Sar asili yake kubwa iko kwao Uholanzi na mizizi yake imetoka kwa Ajax Amsterdam ambako alikaa Miaka 9 tangu aanze kucheza Soka la kulipwa na kutwaa Ubingwa wa Uholanzi mara 4, Kombe la Uholanzi mara 3 na mara moja moja Kombe la Ulaya, UEFA Cup, UEFA Super Cup na Kombe la Bara [Sasa ndio Klabu Bingwa Duniani].
Pia, Van der Sar amekiri kuwa Meneja wa sasa wa Ajax, Frank de Boer, ambae ni Mchezaji wa zamani wa Uholanzi, ni rafiki yake mkubwa kwa zaidi ya Miaka 20.
Lakini, Edwin van der Sar amenena: ‘Ingawa naomba Frank de Boer apate matokeo anayotaka lakini naamini Familia yote ya van der Sar ni Mashabiki wakubwa wa Man United!’

No comments:

Post a Comment