Subscribe:

Ads 468x60px

KIPONDO 4-0 SAN SIRO: Wenger akiri: ‘Ni maafa, ni siku mbaya mno kwetu Ulaya!


Arsene Wenger 


Arsene Wenger amekubali kipondo cha bao 4-0 walichokipata San Siro mbele ya Mabingwa wa Italia AC Milan kwenye mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kimemaliza matumaini yao kwenye mashindano hayo na amekiri yalikuwa matokeo ya kustua na uchezaji wao uliwastua zaidi.
Aliungama: ‘Ulikuwa usiku mbaya kwetu ambao hausahauliki. Ni Usiku mbaya mno kwetu kwa Ulaya. Tumeadhibiwa na tulistahili. Nahisi hatukuwa kwenye gemu, tulikuwa wadhoofu kushambulia na kujilinda. Inastua lakini tulishindwa kila idara uwanjani!’
Wenger aligoma kuongea zaidi na kusema bora akae kimya wajipange upya kwa mechi ijayo ya FA Cup ambayo ipo Jumamosi na wapo ugenini Stadium of Light kucheza  na Sunderland ambao Wikendi iliyopita Uwanja huo huo Arsenal walishinda bao 2-1 kwenye mechi ya Ligi huku bao la ushindi likifungwa na Thierry Henry dakika ya mwisho lakini mechi hii ijayo Henry hayupo tena kwa vile mkopo wake  umeshaisha na yupo njiani kurudi Klabuni kwake New York Red Bulls huko Marekani.
Akiongelea kwenye mtandao wa Twitter, Nahodha wa zamani wa Arsenal, Patrick Viera, alisema: ‘Kulikuwa hamna uongozi uwanjani. Huwezi kumlaumu Arsene peke yake lazima Wachezaji wawajibike!’
Na Wenger mwenyewe amesema: ‘Kuna hatari matokeo haya yatatuumiza kwenye Ligi. Inabidi tufanye kazi ya ziada kujizatiti upya na hatuna muda mrefu kwa mechi ya Jumamosi. Inabidi tuonyeshe kitu tofauti siku hiyo.
Habari kwa Hisani ya : http://www.sokainbongo.com

No comments:

Post a Comment