Subscribe:

Ads 468x60px

TORRES ACHEZA MECHI YA 20 - AKIWA DIMBANI KWA DAKIKA 1298 BILA GOLI HUKU CHELSEA WATOKA SARE NA BIRMINGHAM CITY.


Fernando Torres sasa amecheza mechi ya 20 bila kufunga bao kwa timu yake ya Chelsea. Torres ambaye alitolewa half time na nafasi yake kuchukuliwa na Drogba – sasa ameanza kujihakikishia nafasi yake katika listi ya wachezaji ambao Chelsea walitumia pesa nyingi kuwanunua lakini wakashindwa kuperform vizuri.

 Katika mechi  hiyo ya kombe la FA Cup raundi ya tano dhidi ya Birmingham City, El nino amefikisha idadi ya dakika 1298 akiwa kavaa jezi ya Chelsea bila kuwa na goli.
Torres sasa anaongezeka katika listi inayowajumuisha wachezaji wengine walionunuliwa na Chelsea kwa bei mbaya lakini wakashindwa kufanya vizuri kama vile Andrain Mutu, Mateja Kezman, Andry Shevchenko na hataChris Sutton  kama worst signings of Chelsea ever.

No comments:

Post a Comment