Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Congo DR, Claude Le Roy, amewasili jana Jijini Dar es Salaam akitokea Paris, Ufaransa na Msafara kamili wa Watu 24 wakiwemo Wachezaji 19 wa Timu ya Congo DR utaingia Nchini hapo Jumanne Februari 21 kwa ajili ya Mechi yao ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo Alhamisi Februari 23.
Claude Le Roy, Raia wa Ufaransa, aliteuliwa kuwa Kocha wa Congo Septemba Mwaka jana na huko nyuma aliwahi pia kuwa Kocha wa Senegal, Ghana na Cameroun.
Taarifa hiyo ya TFF pia ilisema Makocha Jan Poulsen wa Taifa Stars na Claude Le Roy watakuwa na Mkutano na Wanahabari hapo Februari 22 utakaofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya TFF.
http://www.sokainbongo.com/dimbani-afrika/2470-stars-v-congo-kocha-wa-congo-atua-dar-timu-kuingia-jumanne
http://www.sokainbongo.com/dimbani-afrika/2470-stars-v-congo-kocha-wa-congo-atua-dar-timu-kuingia-jumanne
Mechi hii na Congo DR ni ya majaribio na matayarisho kwa Taifa Stars ambao wanakabiliwa na mechi ya kuwania kutinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini Mwaka 2013 dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Februari 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kurudiana huko Maputo hapo tarehe 17 Juni 2012.
No comments:
Post a Comment