Kwa siku nzima ya jana mtuhumiwa wa mauaji ya muigizaji maarufu nchini Steven Kanumba,Elizabeth `Lulu`Michael alikuwa amegoma kuongea chochote juu ya siri anayoijua ya kifo cha msanii huyo.
Hatimaye Lulu ameamua kuuvunja ukimya na kuwaeleza polisi nini kilikuwa kimetokea hadi kupelekea kifo cha Kanumba.Katika taarifa aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari,kamanda wa polisi wa mkoa wa kinondoni Afande Charles Kenyela amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Kanumba alikunywa pombe aina ya whisky inayokwenda kwa jina la `Jack Daniels`lakini hakufafanua kwa kiwango kipi kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea na hiyo ni taarifa ya awali tu.
Kuhusu Lulu Afande Kenyela amesema wamefanikiwa kumuhoji binti huyo mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 18 na katikamaelezo yake binti huyo amesema yeye hakuwa amemsukuma marehemu.Vyombo vingi vya habari jana vilimnukuu ndugu wa marehemu Kanumba Seth akisema kuwa Lulu alimsukuma marehemu kabla ya kifo chake.
Kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda Kenyela alisema kwamba ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu.
“Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa
nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa
akizungumza na mwanaume mwingine.
Baada ya Lulu kuona Kanumba anamfuata,Lulu aliamua kukimbia kutoka nje ya geti,lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema Kamanda huyo.
Akiendelea kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango,alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini,”alisema.
Mwisho Kamanda Kenyela alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.

No comments:
Post a Comment