Subscribe:

Ads 468x60px

POULSEN ATAJA STARS WATAKAO IVAA MSUMBIJI


KOCHA MKUU WA TAIFA STARS



Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Jan Poulsen, ametangaza majina ya Wachezaji 23 watakaoingia kambini kujitayarisha kwa mechi ya mchujo kutinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini Januari Mwakani dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Dar es Salaam hapo Februari 29.
Kikosi hicho ambacho kitaingia kambini Februari 20 kina Wachezaji wapya wawili ambao ni Jonas Gerald wa Simba na Salum Abubakar wa Azam.
Kikosi hicho cha Taifa Stars inategemewa kucheza mechi ya kirafiki ya Kimataifa na Congo DR Februari 23 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kikosi kamili:
Makipa: Shabani Kado [Yanga], Juma Kaseja [Simba], Mwadini Ali [Azam]
Mabeki: Shadrack Nsajigwa [Yanga], Masoud Cholo [Simba], Aggrey Morris [Azam], Juma Nyosso [Simba], Juma Jabu [Simba], Stephen Mwasika [Yanga], Kelvin Yondani [Simba]
Viungo: Jonas Gerrard [Simba], Shaban Nditi [Mtibwa Sugar], Shomari Kapombe [Simba], Salum Abubakar [Azam], Mwinyi Kazimoto [Simba] Abdi Kassam [Azam]
Mafowadi: Hussein Javu [Mtibwa Sugar], John Bosco [Azam], Nizar Khalfan [Philadelphia Union, Marekani], Mrisho Ngassa [Azam], Ally Badru Ally [Canal Suez, Misri], Uhuru Selemani [Simba], Nsa Job [Villa Squad].

No comments:

Post a Comment