Subscribe:

Ads 468x60px

RONALDO AFIKISHA MAGOLI 100 MAPEMA ZAIDI KULIKO MCHEZAJI YOYOTE KATIKA HISTORIA YA LA LIGA

Cristiano Ronaldo ndie mchezaji aliefikisha magoli 100 mapema zaidi katika historia ya La Liga.Alifikia rekodi hiyo jumamosi ya mwisho wa wiki iliyopita wakati Real Madrid walipoisambaratisha Real Sociedad kwa mabao 5-1.Imemchukua mechi 92 tu kufikia rekodi hiyo na kumpiku aliekuwa anashikilia rekodi hiyo Ferenc Puskas ambaye ilimchukua mechi 105 kufikia magoli 100
Kuna rekodi nyingine ambayo Ronaldo anakaribia kuivunja.Iwapo atakuja kuifunga bao Barcelona na Real Mallorca, atakuwa ni mchezaji wa kwanza kwenye La Liga kuipiga bao kila timu aliyocheza nayo kwenye msimu mmoja.Ronaldo hajafanikiwa kuifunga Barcelona wala Mallorca msimu huu

No comments:

Post a Comment