Subscribe:

Ads 468x60px

WACHEZAJI 20 WA CONGO WAZAMA NA KUFA MAJI

Wachezaji 20 wa timu moja ya Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo iitwayo AC Virgin KA wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama kwenye mto Luapula nchini Zambia
Kwa mujibu wa kamishna msaidizi wa polisi wa wilaya ya Luapula, Aaron Mushanga,wachezaji hao na washabiki wao  walikuwa wakirejea kutoka Zambia walikokuwa  wakicheza mechi ya mpira wa miguu dhidi ya timu moja ya Zambia ambayo ilichezwa jumapili mwishoni mwa wiki iliyopita,ambapo boti zote tatu walizokuwa wakisafiria zilipinduka na kuzama katika mto maarufu mjini Luapula

"Boti zao zilipinduka katikakati ya mto na kuzama baada ya kupigwa na wimbi lililoanzishwa na boti nyingine iliyokuwa ikipita njia"Alisema Bw. Mushanga
 "Boti zilizozama zilikuwa zimebeba jumla ya watu 100,lakini 80 kati yao waliweza kuokolewa na waokozi na 20 waliangamia"Aliongeza
Ilipofika jumanne wakazi wa mji huo walikuwa wakihangaika kuziopoa boti hizo huku polisi wasimamia utambuzi wa maiti,Rais wa FIFA Sepp Blatter ametuma salam za rambirambi kwa Shirikisho la Soka la Kongo
"Kwa niaba ya FIFA na mimi binafsi, napenda kuwapa pole sana pole  Shirikisho la Soka la Kongo" Blatter aliandika katika ujumbe ali mtumia Constant Omari Selemani,rais wa shirikisho la soka la Kongo FECOFA

No comments:

Post a Comment