Mshambuliaji wa Manchester City Mario Balotelli amepata ajali ya gari
jana alhamisi mchana,lakini taarifa zilizothibitishwa na klabu yake
zimesema kuwa Balotelli alinusurika na wala hakupata majeraha yoyote
Mshambuliaji huyo alikuwa akiendesha gari yake aina ya Bentley
alipogongana na gari nyingine kwenye mtaa mmoja uitwao Medlock jijini
Manchester.Klabu yake imesema kuwa Balotelli hakuwa mwenye makosa lakini polisi wa Greater Masnchester wanafanya uchunguzi kujua chanzo cha ajali.Polisi wamesema kwenye taarifa yao kuwa mtu mmoja kutoka katika gari zilizohusika na ajali amekimbizwa hospitali kwa tahadhali
No comments:
Post a Comment