Subscribe:

Ads 468x60px

TERRY APASUKA MBAVU



Chelsea imethibitisha kuwa nahodha wao John Terry amepata mipasuko kwenye mbavu zake na watakuwa wakifuatilia hali yake kwa karibu kabla ya mechi zinazofuata.
Terry alitoboa siri jana kuwa anapata shida kupumuaa wakati anacheza,baada ya kuumia katika mechi ya kwanza na Benfica wiki ilyopita ila alimudu kucheza dakika zote 90 jumamosi iliyopita katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Aston Villa.Lakini katika mechi ya Uefa jumatano alidumu uwanjani kwa dakika 60 tu na baadae alitolewa.
Asubuhi ya jana alhamisi vipimo vya scan vilionesha kuwa Terry amepasuka mbavu mbili.Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa klabu wa www.chelseafc.com Chelsea wamesema wamefanikiwa kulishughulikia tatizo na watamwangalia mlinzi wao huyo wa kutegemewa kwa ukaribu zaidi kabla ya mechi zinazofuata

No comments:

Post a Comment