Subscribe:

Ads 468x60px

MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA ANDRE VILLAS-BOAS DARAJANI


Andre Villas-Boas yupo katika mgumu kuliko wakati wowote katika maisha yake ya ukocha @Chelsea.

Siku kadhaa baada ya mafaza wa Chelsea kumchallenge katika kikao cha timu hiyo,
AVB tena alilazimika kukanusha taarifa mpya kwamba Didier Drogba aliwaweka kikao kifupi wachezaji wenzake wakati wa mapumziko wa mechi ya raundi 5 ya FA Cup dhidi ya Birmingham.
Mreno huyo alipinga taarifa zilizotoka kuhusu kikao cha Drogba na wenzie huku akiweka na kukiri kwamba Fernando ‘Flop’ Torres aliangalia kipindi cha pili katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kutolewa wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Drogba.

Akizungumzia sub ya Torres AVB alisema: “Nina uhakika Torres hakupenda kutolewa muda ule lakini yalikuwa ni maamuzi kwa faida ya timu.”

Chelsea wanasafiri kwennda Napoli wiki hii kwa ajili ya mechi ya kwanza ya mtoano wa Champions league, huku taarifa zikisema atatimuliwa ikiwa Chelsea watshindwa kuingia robo fainali.

Pia AVB sasa ameshaanza kukosa support ya mashabiki wa Chelsea baada ya wapenzi wa timu hiyo sasa kuanza kuimba jina la Jose Mourinho katika mechi za Chelsea huku wakiizomea timu yao muda wote.
Drogba Akiendesha kikao na wachezaji wenzie wakati wa mapumziko.

MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU EMIRATES: ARSENAL WAPIGWA 2-0 NA SUNDERLAND WATOLEWA FA CUP.

Kieran Richadson akipongezwa na wenzie.

Mambo yameendelea kuwa magumu kwa Arsenal baada ya leo pia kutolewa katika michuano ya kombe la FA na Sunderland baada ya kufungwa 2-0 na watoto wa Martin O’neal.
Magoli ya Sunderland yalifungwa kwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United Kieran Richdson katika dakika ya 48 kabla ya Alex Oxlade Chamberlain akijifunga na kufunga idadi yam abo ya mchezo huo wa raundi ya tano ya FA.
 Wiki hii imeendela kuwa mbaya kwa Arsenal ambao walifungwa kwa goli 4-0 na AC Milan katika mechi ya kwanza ya Champions league.

TORRES ACHEZA MECHI YA 20 - AKIWA DIMBANI KWA DAKIKA 1298 BILA GOLI HUKU CHELSEA WATOKA SARE NA BIRMINGHAM CITY.


Fernando Torres sasa amecheza mechi ya 20 bila kufunga bao kwa timu yake ya Chelsea. Torres ambaye alitolewa half time na nafasi yake kuchukuliwa na Drogba – sasa ameanza kujihakikishia nafasi yake katika listi ya wachezaji ambao Chelsea walitumia pesa nyingi kuwanunua lakini wakashindwa kuperform vizuri.

 Katika mechi  hiyo ya kombe la FA Cup raundi ya tano dhidi ya Birmingham City, El nino amefikisha idadi ya dakika 1298 akiwa kavaa jezi ya Chelsea bila kuwa na goli.
Torres sasa anaongezeka katika listi inayowajumuisha wachezaji wengine walionunuliwa na Chelsea kwa bei mbaya lakini wakashindwa kufanya vizuri kama vile Andrain Mutu, Mateja Kezman, Andry Shevchenko na hataChris Sutton  kama worst signings of Chelsea ever.

Stars v Congo: KOCHA wa Congo atua Dar, Timu kuingia Jumanne


Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Congo DR, Claude Le Roy, amewasili jana Jijini Dar es Salaam akitokea Paris, Ufaransa na Msafara kamili wa Watu 24 wakiwemo Wachezaji 19 wa Timu ya Congo DR utaingia Nchini hapo Jumanne Februari 21 kwa ajili ya Mechi yao ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo Alhamisi Februari 23.
Claude Le Roy, Raia wa Ufaransa, aliteuliwa kuwa Kocha wa Congo Septemba Mwaka jana na huko nyuma aliwahi pia kuwa Kocha wa Senegal, Ghana na Cameroun.
Taarifa hiyo ya TFF pia ilisema Makocha Jan Poulsen wa Taifa Stars na Claude Le Roy watakuwa na Mkutano na Wanahabari hapo Februari 22 utakaofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya TFF.
http://www.sokainbongo.com/dimbani-afrika/2470-stars-v-congo-kocha-wa-congo-atua-dar-timu-kuingia-jumanne
Mechi hii na Congo DR ni ya majaribio na matayarisho kwa Taifa Stars ambao wanakabiliwa na mechi ya kuwania kutinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini Mwaka 2013 dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Februari 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kurudiana huko Maputo hapo tarehe 17 Juni 2012.


WAGHANA HAWANA SHUKRANI...

Emmanuel agyemang Badu


Ikiwa ni siku moja tu tangu mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana,Asamoah Gyan atangaze kustaafu soka la kimataifa,mchezaji mwenzie katika timu ya taifa ambaye anachezea Udinese ya Italia Emmanuel agyemang Badu amesema waghana hawaheshimu juhudi zinazofanywa na wachezaji wa Black Stars
Akiongea na mtandao wa footy-ghana.com,Badu amesema kashtushwa sana na taarifa za kustaafu kwa Gyan na pia amesikitishwa na kitendo cha washabiki wa Ghana kuimiminia matusi makali familia ya Gyan tangu baada ya tukio la kukosa penati kwenye michuano ya kombe la mataifa ya afrika
"matusi yamezidi,waghana hawatambui mchango wa Gyan katika timu ya taifa,yeye ndie mfungaji anaeongoza katika timu yetu,hivyo hii ni habari mbaya kwa Ghana.Familia yake haikustaili matusi yote hayo"

Asamoah Gyan astaafu Ghana!



Straika wa Ghana Asamoah Gyan inasemekana ameamua kupumzika kuichezea Ghana baada ya kutuma barua kwa Chama cha Soka Ghana, GFA, akielezea uamuzi wake huo.
Gyan, Miaka 26, ambae ameichezea Ghana mara 59, ameleza kuwa uamuzi wake huo unatokana na kukashifiwa vibaya mara baada ya Ghana kubwagwa nje toka kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2012, hivi majuzi walipofungwa bao 1-0 na Zambia.
Mchezaji huyo amekuwa akisakamwa mno Nchini kwao kwa kuwaletea maudhi makubwa kwa kukosa penati kwenye mechi ya AFCON 2012 dhidi ya Zambia na pia kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay huko Afrika Kusini Mwaka 2010.
Barua hiyo ya Gyan imeeleza kuwa uamuzi wake hakuuchukua kwa mzaha na anasikia fahari kubwa kuichezea Ghana tangu akiwa na Miaka 17 Mwaka 2003.
Akimalizia barua yake, Gyan, ambae sasa anacheza kwa mkopo huko UAE na Klabu ya Al Ain toka Sunderland, amesema ataijulisha GFA akiamua kurudi tena kuichezea Ghana.
Gyan ameifungia Ghana bao 28 katika Mechi 59 alizoichezea.

ZLATAN IBRAHIMOVIC: VAN PERSIE ONDOKA ARSENAL




Robin Van Persie ameambiwa na Zlatan Ibrahimovic aondoke Arsenal kama anataka kushinda vikombe.

Nahodha wa gunners alishindwa kuisadia timu yake juzi Jumatano wakatika Gunners walipopewa kipigo cha 4-0 na AC Milan na kuweka matumaini finyu ya kuendelea na hatua ya mbele katika champions league.

Akiongea na The Sun Zlatan alisema: “Inapofikia kipindi hujashinda kombe lolote kwa miaka mingi watu wanaelewa unapoondoka kama Cesc Fabregas. Soka ni kila kitu kuhusu kushinda. Kama usiposhinda inabidi uondoke. Simjui kiundani Robinlakini nakumbuka jinsi alivyokuwa na kipaji kikubwa tangu akiwa Uholanzi – na sasa amekamilika.
“Sijui nini anafikiria kuhusu hatma yake kisoka lakini ningekuwa mimi ningejua cha kufanya tayari. Nimeshahama sana katika maisha yangu ya soka – nachukulia suala kama changamoto ya kufanya vizuri kwangu. Na nimeshashinda makombe 8 katika miak 8 na klabu tofauti katika nchi mbalimbali.
“Lakini kama utakaa sehemu moja katika maisha yako yote ni rahisi kucheza soka, unajihisi kama upo nyumbani na katika zone ambayo unakuwa comfortable kucheza soka., lakini ikiwa unahama katika sehemu tofauti inakuwa ni tofauti ni kama mtihani. Ikiwa utafanikiwa hapo ndipo unapokuwa bingwa wa kweli na hapo ndipo utakapopata heshima.”

SIMBA NAO WATOKA SARE NA KIYOVU KIGALI RWANDA





Wawakilishi wa Tanzania Bara katika kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) Simba SC imetoa sare ya goli 1-1 na Kiyovu ya Rwanda mchezo uliochezwa nchini Rwanda.

Simba walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa kiungo Mwinyi Kazimoto katika dakika ya 42 ya mchezo, na kupelekea Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli hilo moja.

Wakati mashabiki wa Kiyovu wakiwa wameshakubali matokeo ya kufungwa goli moja bila, na kuanza kutokomea uwanja katika dakika ya 90 walisazisha goli hilo na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Simba na Kiyovu watarejeana tena baada ya wiki mbili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na matokeo hayo ya leo yanawapa hauweni Simba katika mchezo wa marudiano kwani watahitaji sare ya bila kufungana.

YANGA YATOKA SARE NA ZAMALEK TAIFA - AMRI ZAKI AINYIMA USHINDI

Klabu ya Dar Young African leo imeshindwa kuifunga Zamalek ya Misri kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wa Afrika baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja.
Katika mchezo huo ambao Yanga waliutawala kwa kiasi kikubwa huku Zamalek wakicheza kwa kijihami na kufanya mashambulizi ya kushtukiza, wanajangwani itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kupoteza nafasi nyingi za magoli ya wazi.



Yanga ndio walikuwa wa kwanza kuzitingisha nyavu za Zamalek kwa goli lilofungwa na Hamis Kiiza katika kipindi cha kwanza kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Wigan Athletic Amri Zaki aliyeingia akitokea benchi kuisawazishia Zamalek. wa marudiano dhidi ya Waarabu hao utakaopigwa wiki 2 zijazo katika venue ambayo bado haijawekwa wazi.
Kwa matokeo hayo ni dhahiri Yanga wamejiweka katika wakati mgumu atika mchezo

Nini hasa tatizo kubwa kwa TIGER HOOD kuporomoka kwa kiwango chake cha GOLF?


Nini hasa tatizo kubwa kwa TIGER HOOD kuporomoka kwa kiwango chake cha GOLF? 
JE NI baada ya kuachana na wife wake kwa SKENDO za mapenzi au kachoka kabisa?Nani mwenye kufahamu hili jambo wadau.


    • Iddy Harnaa Mkwama :Skendo zimemshusha sana

    • Carlos Nkwera: Tatizo kubwa linalomfanya ashuke ni skendo zilizomwandama

    • Faraji Makay :gemu inakupanda na kushuka...vile m2 awezi kuwa juu muda wote...!!!
    • Gulam Mhedu :Umaarufu mzigo wa miba, halafu kuwa number moja kwa muda inawezekana ila kukaa hapo milele haiwezekani!

    • Rajabu Abeid: Kila jambo lina msimu.


    • Wence Mapunda :Hamna WAZUNGU wamemshusha kiwango walianza na MUHAMAD ALI kipindi kile mara aende jeshini. Wakaja kwa MIKE TYSON na yy wakamfanya hivhiv na sasa wamehamia kwa TIGER WOODS sasa wazungu ndio wanamuua kabisa ila naamini akituliza

    • Linus Anthony: Me nadhan ni kuchoka coz ata masupa* wa soka wanaishaga mdogo mdogo

    • Adamu Said :Gem imemfua skendo ni sabab
    • Mkusa Mancho: Mbele siku zote wadhamini ndo kla kitu achana na mshahara unaopata so wanaamini kuwa maarufu ni mfano ktk jamii ukifanya ktu ambacho kitaharibu heshima yako kma alivyofanya Tiger Woods wadhamini wanavunja mikataba yao unaporomoka kiuchumi matumizi yako yanashuka na mbele kuna haki nyingi zinawabeba wanawake so asilimia kubwa ya utajiri wako unakwenda kwa mkeo unachanganyikiwa kiwango kinashuka vilevile kwa mawazo. So unatakiwa uwe mwangarifu unapokuwa superstar especially ukiwa umeoa kuna haki nyingi za wanawake mbele usipoangalia dunia utaiona chungu@Ingram

CAF AFRIKA: Yanga v Zamalek; Kiyovu v Simba

YANGA_V_SIMBA11Klabu kongwe Nchini, Yanga na Simba, Leohii zinajimwaga dimbani kwenye Mashindano makubwa Barani Afrika huku Yanga wakiikaribisha Zamalek ya Misri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo Jumamosi kwa pambano la Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Simba kucheza ugenini, pia Jumamosi, huko Kigali, Rwanda na Kiyovu kwenye Kombe la Shirikisho.
Mbali ya wakongwe hawa, Timu za Zanzibar, Mafunzo na Jamhuri, nazo zitaingia uwanjani kwa Mafunzo kucheza na Liga Muculmana de Maputo ya Msumbiji katika CAF CHAMPIONZ LGI na Jamhuri kuivaa Hangwe ya Zimbabwe kwenye Kombe la Shirikisho.
Tayari Zamalek, ambao wamewahi kuwa Mabingwa wa Afrika mara 5, wameshatua Dar es Salaam bila ya Wachezi wao Ahmed Hassan, Muhammad Ibrahim na Salah Suleiman.
Majuzi Zamalek walicheza mechi yao ya mwisho ya majaribio na kuifunga Telecom Egypt bao 4-1 kwa bao za Amr Zaki, Ibrahim Hassan na Ahmad Jaffar.
Simba yaenda Rwanda bila Wachezaji kadhaa
Simba iliondoka Alhamisi jioni kwenda Kigali, Rwanda kupambana na Kiyovu huku Wachezaji kadhaa wakiachwa.
Wachezaji ambao hawakusafiri ni Gervais Kargo, Derrick Walulya, Haruna Moshi 'Boban', Ulimboka Mwakingwe, Amir Maftah na Hassan Khatib na imesemwa baadhi yao ni majeruhi.
Pamoja na Kocha Cirkovic Milovan na Wasaidizi wake Amatre, Daktari Cosmas Kapinga na James Kisaka, Kocha wa Makipa, Viongozi wengine ambao wamo kwenye msafara huo ni Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange 'Kaburu', Katibu mkuu Evodius Mtawala, Fransis Silaya (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji).
Wachezaji waliosafiri ni:
Makipa: Juma Kaseja na Ali Mustapha 'Barthez'
Mabeki: Nassor Said 'Cholo', Juma Jabu, Juma Nyoso, Kelvin Yondan, Victor Costa na Obadia Mungusa.
Viungo: Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Patric Mafisango Washambuliaji: Ramadhani Singano 'Messi', Edward Christopher, Salum Machaku, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Emmanuel Okwi.

MISIMAMO & RATIBA LIGI ZA ULAYA:

LA LIGA
MSIMAMO=Timu za juu tu:
[Kila Timu imecheza Mechi 22]
1 Real Madrid Pointi 58
2 Barcelona 48
3 Valencia 40
4 Levante 32
5 RCD Espanyol 32
6 Atletico de Madrid 31
7 Malaga 31
8 Osasuna 31
9 Athletic de Bilbao 30
10 Rayo Vallecano 28

SERIE A
MSIMAMO=Timu za juu tu:
[Kila Timu imecheza Mechi 23 isipokuwa inapotajwa]
1 AC Milan Pointi 47
2 Juventus Mechi 22 Pointi 46
3 Lazio 42
4 Udinese 41
5 Napoli Mechi 24 Pointi 37
6 Inter Milan Mech 24 Pointi 35
7 AS Roma 35
8 Palermo 31
9 Cagliari 30
10 Genoa 30

BUNDESLIGA
MSIMAMO=Timu za juu tu:
[Kila Timu imecheza Mechi 21 isipokuwa inapotajwa]
1 Borussia Dortmund Pointi 46
2 Bayern Munich 44
3 Borussia Monchengladbach 43
4 Schalke 41
5 Werder Bremen 33
6 Bayer Leverkusen 31
7 Hannover 31
8 Wolfsburg 27
9 Stuttgart 26
10 Hoffenheim Mechi 22 Pointi 26

RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Februari 17
SERIE A
Forentina 0 Napoli 3
Inter Milan 0 Bologna 3
BUNDESLIGA
Hoffenheim 1 Mainz 1
Jumamosi Februari 18
LA LIGA
Getafe v Espanyol
Real Madrid v Real Racing Santander
Sevilla v Osasuna
SERIE A
Juventus v Catania
BUNDESLIGA
Kaiserslautern v Borussia Monchengladbach
Nuremberg v Cologne
Bayer Leverkusen v Augsburg
Hamburger v Werder Bremen
Hertha Berlin v Borussia Dortmund
Freiburg v Bayern Munich
Jumapili Februari 19
LA LIGA
Granada v Real Sociedad
Athletic Bilbao v Malaga
Real Mallorca v Villareal
Sporting Gijon v Atletico Madrid
Levante v Rayo Vallecano
Barcelona v Valencia
SERIE A
Lecce v Sienna
AS Roma v Parma
Genoa v Chievo
Cesena v AC Milan
Novara v Atalanta
Udinese v Cagliari
Palermo v Lazio
BUNDESLIGA
Schalke v Wolfsburg
Hannover v Stuttgart

Facebook status: "Leo nakunywa mayai sauti iwe nyororo tayari kwa kuishangilia ZAMALEK...uzalendo my foot" says Soggy Dog


Leo nakunywa mayai sauti iwe nyororo tayari kwa kuishangilia ZAMALEK...uzalendo my foot



 ·  ·  · 26 minutes ago · 

  • 7 people like this.

    • Elliude Pemba Tunasubiri kuwaona wanapigwa 4 saaafi.
      15 minutes ago · 

    • Dravic Moudy HAHAHAHA' YANGA 0 ZAMALEK 5' AFU YANGA NI VIRUS NAO WANAPEWA PROMO N WALE JAMAA
      15 minutes ago · 

Guyz naombeni mnisaidie eti HASHIM THABIT anacheza timu gani


Guyz naombeni mnisaidie eti HASHIM THABIT anacheza timu gani?

    • Amosy Morchy Kibangali Memphis grillerz
      8 hours ago via mobile ·  ·  1

    • Andy Mapunda Chelsea Asante amos.dah huyu jamaa bora arudi2 nyumbani maana huko achez.
      8 hours ago via mobile · 

    • Kijo Madeleka Hasheem Thabit alichukuliwa na Memphis Grizzlies kutoka College. Hawakuridhika na mwenendo wa kiwango chake wakampeleka timu ya Dakota Wizard katika D-League (Development League) ili akapate uzonefu na aweze kucheza vizuri NBA. Huko alifanya vizuri wakamrudisha kucheza NBA lakini bado akashindwa kuwaridhisha Memphis wakaamua kumuuza Houston Rockets huko napo hakuweza kuonyesha kiwango na wamempeleka tena D-League ili apate uzoefu na kuongeza kiwango. Kwa hiyo hadi sasa Hasheem ni mchezaji wa Houston Rockets lakini kwa sasa anachezea Rio Grande Valley Vipers ktk D-league.
      Hayo ndo maelezo machache kuhusu ndugu yetu Hasheem Thabit naamini utakuwa umenipata fresh mdau Andy Mapunda Chelsea

      7 hours ago ·  ·  2

    • Andy Mapunda Chelsea Nimekupata kijo thax.